Aug 08, 2018 14:40 UTC
  • Zarif: Dunia haiafikiani na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran + Video

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, dunia haiafikiani na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema kuwa, sasa hivi nchi mbalimbali duniani zinafanya juhudi za kupambana na vikwazo hivyo.

Muhammad Javad Zarif amesema hayo leo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa, Marekani haina mwamana hata kidogo. Amesema, kama ambavyo madai ya Donald Trump ya kwamba eti anapenda kuwa na mazungumzo na Iran, hayana maana yoyote, ni vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa madai ya Wamarekani ya kuiwekea mashinikizo Iran, nayo hayamshughulishi mtu.

 

Amesisitiza kuwa, kamwe Wamarekani hawajawahi kuwa na nia njema katika mazungumzo yao na Iran na ndio maana pendekezo la Trump la kuwa na mazungumzo na Iran ikahesabiwa kuwa ni hatua ya kipropaganda tu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebainisha kuwa, moja ya ushahidi unaothibitisha kuwa Trump ni adui mkubwa wa wananchi wa Iran ni kwamba vikwazo vya kwanza kabisa vilivyowekwa na rais huyo wa Marekani dhidi ya Iran ni vya ndege za abiria.

Rais wa Marekani, Donald Trump

Amma kuhusiana na mazungumzo baina ya Iran na nchi za Ulaya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA, Zarif amesema, nchi za Ulaya hazipaswi kutosheka tu na ahadi zao za maneno, bali zinapaswa kugharamia ulinzi na utekelezaji wa mapatano hayo.

Siku ya Jumatatu tarehe 6 Agosti, rais wa Marekani, Donald Trump alitoa amri ya kurejeshwa vikwazo vilivyo kinyume cha sheria dhidi ya Iran katika sekta za utengenezaji magari na dhahabu.

Tags

Maoni