Aug 13, 2018 02:51 UTC
  • Wakristo wa Iran wamwambia Pompeo: Wafuasi wa dini za wachache Iran hawahitajii usimamizi wa Marekani

Jumuiya ya Wakristo wa Assyrian nchini Iran imejibu ujumbe wa Twitter wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani aliyedai kuwa wafuasi wa dini za waliowachache wanasumbuliwa na kunyimwa haki zao za binadamu hapa nchini kwa kusema kuwa: Wafuasi wa dini za waliowachache nchini Iran hawahitaji usimamizi wa Marekani.

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Jumuiya ya Wakristo wa Assyrian nchini Iran imesema hapana shaka kuwa, machozi ya mamba yaliyotolewa na Mike Pompeo ambaye hadi sasa nchini kwake bado watu wananyanyaswa kwa sababu tu ya rangi ya ngozi zao na utumwa uliofutwa na Abraham Lincoln ungali unafanyika kwa sura nyingine, hayaonekani kuwa ni ya kimantiki na kiadilifu. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kujenga ukuta wa kutenganisha mataifa mawili katika mipaka ya Marekani tena miongo kadhaa baada ya kubomolewa kuta na vizuzi mbalimbali baina ya mataifa na vilevile dhulma ya kuwatenganisha watoto na wazazi wao na kuwashikilia katika kambi zinazoshabihiana na za Manazi za "Auschwitz Concentration", ni kilele cha ukatili na ushenzi katika jamii ya dunia ya leo.

Watoto wadogo wanatenganishwa na wazazi wao wahajiri nchini Marekani.

Taarifa hiyo ya Wakristo wa Assyrian imesisitiza kuwa, wafuasi wa dini za waliowachache nchini Iran wanautambua mfumo wa Kiislamu unaotawala nchini Iran kuwa ni nguzo na msaidizi wao katika kulinda utamaduni, lugha na dini yao.  

Tags

Maoni