Aug 17, 2018 15:42 UTC
  • Sayyid Aboutorabi Fard: Iran inao uwezo wa kukabiliana na njama za kiuchumi za adui

Khatibu wa swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran sambamba na kuashiria njama za adui za kutoa pigo kwa uchumi wa Iran amesisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inao uwezo mkubwa wa kukabiliana na njama za kiuchumi za adui huyo.

Hujjatul-Islami wal-Muslimina Sayyid Mohammad-Hassan Aboutorabi Fard ameyasema hayo katika hotuba ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ambapo akiashiria vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa hili, amesema kuwa, vikwazo hivyo vya Marekani ni fursa kwa ajili ya kuchanua uchumi wa Iran. Aidha amezungumzia mwaka wa kurejea mateka waliokomboka wa Iran hapa nchini na kuongeza kuwa, mateka waliokomboka wa Iran ambao walipitisha uhai wao katika mazingira magumu ya jela za utawala wa Baath wa Iraq, ni wabeba ujumbe wa damu za mashahidi wa Iran.

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Aidha Khatibu wa swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran amebainisha kwamba, miaka minane ya kujitetea kutakatifu kwa taifa la Iran dhidi ya hujuma za utawala wa Baath wa Iraq, kuliijenga nchi katika uga wa kisiasa, kielimu, kiuchumi na kijeshi na kuongeza kuwa, Lebanon, Syria, Iraq, Yemen na Palestina zimepata ilhamu kutokana na kujitetea huko kwa Iran ambapo hii leo nchi hizo nazo zinapambana na tawala za kibeberu duniani.

Maoni