Sep 01, 2018 04:10 UTC
  • Mazungumzo ya Dakta Zarif na Waziri Mkuu wa Pakistan

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo na Imrah Khan Waziri Mkuu wa Pakistan aliyechaguliwa hivi karibuni.

Dakta Muhammad Javad Zarif ameashiria katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jana (Ijumaa) mjini Islamabad juu ya umuhimu na udharura wa kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan katika nyanja mbalimbali kama mipaka, biashara na uchumi na kusisitiza juu ya udharura kujikurubisha zaidi nchi za Kiislamu katika masuala yanayohusiana na Ulimwengu wa Kiislamu na kieneo.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Waziri Mkuu wa Pakistan wamesisitiza katika mazungumzo yao juu ya umuhimu wa kuongezwa juhudi kwa ajili ya kuleta amani na uthabiti kwa nchi zote za eneo la Mashariki ya Kati.

Kadhalika Javad Zarif na Imran Khan wmetoa wito wa kuweko vita vya kweli vya kupambana na ugaidi pamoja na makundi yenye misimamo ya kufurutu ada.

Dakta Zarif katika mazungumzo yake na Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan

Kabla ya mazungumzo yake na Imran Khan, Dakta Zarif alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Pakistan akiwe Shah Mehmood Qureshi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni, Qamar Javed Bajwa, kamanda wa kikosi cha nchi kavu na Asad Qaiser, Spika wa Bunge la Pakistan.

Dakta Muhammad Javad Zarif aliitembea Pakistan Alkhamisi na Ijumaa akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran kwa shabaha ya kwenda kufanya mazungumzo na viongozi wa serikali mpya ya nchi hiyo lengo likiwa na kupanua zaidi ushirikliano baina ya nchi mbili hizo.

Tayari Dakta Muhammad Javad Zarif amesharejea hapa Tehran baada ya kukamilisha safari yake ya siku mbili nchini Pakistan.

Tags

Maoni