Sep 08, 2018 08:15 UTC
  • Rais Rouhani: Iran haina adui yeyote zaidi ya Marekani, Israel na vibaraka wao

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba, hii leo Iran haina adui mwengine yeyote isipokuwa Marekani, utawala wa Kizayuni na vibaraka wao, amesisitiza kwamba, taifa la Iran litawashinda maadui kwa mshikamano na umoja.

Rais wa Iran ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya 14 ya Tamasha la Kitaifa la Shahidi Rajai mjini Tehran na kubainisha kwamba raia wa Iran kamwe hawatosalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani. Aidha amefafanua kwamba, taifa la Iran halitatishika kwa mashinikizo ya kundi jipya tawala katika ikulu ya Marekani ya White House ambalo watu wake hata wao wenyewe pia hawafahamu nini wanachokisema na wanachokifanya huku wakigombana na kupapurana na nchi zote.

Pande tatu zinazoendesha chuki dhidi ya Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kundi jipya ambalo liko katika ikulu ya Marekani kwa sasa, haliushambulii Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pekee, bali linawashambulia pia marafiki wa zamani na wa jadi wa Washington, na nchi ambazo zina mahusiano mengi ya kiuchumi na nchi hiyo. Akibainisha kwamba kwa upande mmoja Marekani inaliwekea mashinikizo taifa la Iran na kwa upande mwingine inatoa ujumbe wa kufanya mazungumzo, Rais Rouhani amesema kuwa, Wamarekani wana miamala ya undumakuwili na hii leo wanaendesha vita vya kiuchumi na propaganda.

Tags

Maoni