Sep 12, 2018 14:01 UTC
  • Rais Rouhani: Hivi sasa Marekani iko katika hali mbaya sana duniani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba ukiachilia nchi na tawala chache zinazojulikana katika eneo la Mashariki ya Kati ambazo ziko pamoja na Washington, Marekani iko katika hali mbaya zaidi duniani.

Rais Rouhani ameyasema hayo Jumatano ya leo katika kikao cha serikali na kuongeza kuwa, hii leo waitifaki wa Marekani hawako pamoja na nchi hiyo na kwamba hata marafiki wake wa zamani na wa jadi nao wamejitenga na kujifakharisha kuwa mbali na nchi hiyo ya kibeberu. Aidha Rais wa Iran amefafanua kuwa, hata asasi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), haziko pamoja na siasa za Marekani.

Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ameiweka pabaya nchi yake

Kadhalika Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kwamba hali ya sasa ya ndani nchini Marekani inatofautiana sana na hali ya miaka iliyopita na kwamba hii leo nchi hiyo inapitia kipindi kigumu sana katika historia yake, na kusema kuwa, hivi sasa watafiti na wanafikra  nchini humo, hawakubaliani na viongozi wa ikulu ya White House huku wengine wakiwaita wazi wazi viongozi hao kuwa ni ndui, suala ambalo ni mara chache sana kushuhudiwa katika historia ya Marekani. Akibainisha kwamba hii leo Iran iko katika vita vya wazi dhidi ya wavamizi, amesisitiza kwamba, bila shaka yoyote taifa la Iran litaibuka mshindi katika vita hivyo.

Tags

Maoni