Sep 23, 2018 07:57 UTC
  • Rouhani: Iran inawafahamu wahusika wa shambulio la Ahvaz, itawafuatilia

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili linawafahamu wahusika wa shambulio la jana la kigaidi mjini Ahvaz, na lina haki ya kuwafuatilia na kuwawajibisha.

Rais Rouhani ameyasema hayo mapema leo kabla ya kuelekea mjini New York kwenda kushiriki mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA na kubainisha kwamba, wale ambao wanajiita watetezi wa haki za binadamu ndio wanaofaa kubebeshwa dhima ya hujuma ya jana iliyoua makumi ya watu.

Rais Rouhani anatazamiwa kurejea nyumbani Jumatano (Septemba 26) baada ya kukamilisha ziara yake ya siku nne mjini New York.

Maombolezo ya mashahidi wa Ahvaz

Katika hatua nyingine, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Idara ya Masuala ya Ulaya ya wizara hiyo jana jioni iliwaita mabalozi wa Uholanzi, Denmark na Uingereza na kuwakabidhi malalamiko ya Tehran kuhusu uwezekano wa nchi zao kuhusika katika shambulizi hilo.

Kundi la kigaidi la al-Ahvaziya ambalo baadhi ya wanachama wake wako katika nchi kadhaa za Ulaya kama vile Uholanzi na Denmark, limekiri kuhusika na hujuma ya jana.

 

Tags

Maoni