Sep 23, 2018 16:00 UTC
  • Iran yalalamikia ripoti mpya ya Marekani kuhusu ugaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, madai yaliyomo kwenye ripoti ya kila mwaka ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu ugaidi ni ya kinafiki kama ilivyokuwa kwa ripoti zote za kila mwaka za wizara hiyo.

Bahram Qassemi amesema hayo leo kujibu ripoti ya kila mwaka ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu ugaidi ambapo ndani yake imetoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema, tuhuma za kipuuzi na zisizo na msingi dhidi ya Iran zilizomo kwenye ripoti hiyo zimetolewa katika hali ambayo ni jana tu, magaidi wanaungwa mkono na Marekani na vibaraka wake walifanya mauaji dhidi ya raia wa Iran mjini Ahwaz na kwamba dunia nzima imeona namna Iran ilivyo muhanga mkubwa wa vitendo vya kigaidi.

Askari polisi wa Iran akimbeba mtoto mdogo wa miaka minne aliyepigwa risasi na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani, Jumamosi, Septemba 22, 2018. Mtoto huyo hakupona, ni miongoni mwa aliouawa shahidi katika jinai hiyo

 

Amesema, siasa za kinafiki na za kindumilakuwili za Mrekani za kutumia vibaya maneno kama vita dhidi ya ugaidi kwa kweli ndizo zinazoongeza vitendo vya kigaidi duniani na kwamba mkakati mkuu wa Mrekani ni kuharibu utulivu na usalama wa nchi nyingine ili ipate uhalali wa kuendeleza ubeberu wake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, Marekani ambayo inaendesha siasa zake kindumilakuwili na kugawa ugaidi mzuri na mbaya ndiyo inayobeba dhima ya kuendelea kushuhudiwa vitendo viovu vya kigaidi duniani hususan Mashariki ya Kati na inapaswa ibebe lawama za vitendo vya kikatili vinavyofanywa na magenge ya kigaidi.

Tags

Maoni