Sep 24, 2018 07:28 UTC
  • Rais Rouhani awasili New York kushiriki mkutano wa UN

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili New York nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria kutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Baada ya ndege yake kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy, Rais Rouhani ambaye alikuwa amezungukwa na waandishi wa habari alisema kuwa, mazingira ya sasa ya Marekani yanaonekana tofauti na ya miaka iliyopita na kwamba Wamarekani wamerudi nyuma na kujiondoa katika mikataba kadhaa ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mkataba wa nyuklia wa JCPOA.

Rais Hassan Rouhani

Safari ya Rais Rouhani nchini Marekani imefanyika siku moja baada ya shambulizi la kigaidi lililofanyika katika mji wa Ahvaz, kusini mwa Iran na kuua makumi ya watu wasio na hatia.

Kabla ya kuuondoa Tehran, Rais Rouhani alisema kuwa Marekani inafanya mikakati ya kuvuruga usalama na amani nchini Iran kwa msaada wa viinchi vidogo mamluki na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejipanga vizuri kukabiliana nao.

Akizungumzia shambulizi la kigaidi la juzi mjini Ahvaz, Rais Rouhani amesema: "Tunawajua waliofanya shambulizi hilo, ni kina nani na wanafungamana na nani." Amesema Marekani ndiyo inayozipa himaya na misaada nchi ndogo na mamluki wake na kuwachochea kufanya uhalifu na jinai kama hizi.

Shambulizi la kigaidi, Ahvaz

Amesema Marekani inafanya jitihada za kuzusha machafuko nchini Iran na kutayarisha mazingira ya kurejea hapa nchini; hii ni ndoto ambayo haitakariri tena na Marekani haitatimiza malengo.  

Tags

Maoni