Nov 17, 2018 08:07 UTC
  • Rais Rouhani ampokea rasmi Rais wa Iraq mjini Tehran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo amempokea rasmi mwenzake wa Iraq, Barham Salih katika makao makuu yake ya Saadabad mjini Tehran.

Rais Barham Salih wa Iraq amewasili Tehran masaa machache yaliyopita akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

Marais hao wawili wameanza mazungumzo mara moja baada tu ya sherehe rasmi za mapokezi. 

Katika safari hiyo ya siku mbili Rais Rouhani na mwenzake wa Iraq watajadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa. Vilevile ujumbe za masuala ya kisiasa, kuuchumi na kiutamaduni za pande hizo zitajadili na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu pande mbili. 

Katika safari hii ya Rais wa Iraq nchini Iran pande hizo mbili zinajadili suala la kuboresha zaidi ushirikiano katika nyanja mbalimbali. 

Rais Barham Salih wa Iraq amewasili Tehran baada ya kuzitembelea nchi tatu za Jordan, Imarat na Kuwait.  

Tags

Maoni