Dec 12, 2018 16:09 UTC
  • China yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Naibu wa Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa ya Shanghai China anayehusika na masuala ya Asia Magharibi na Afrika amelaani vikwazo na vitendo vya chuki vinavyoendeshwa na Marekani dhidi ya Iran.

Jin Liangxiang amesema hayo leo Jumatano wakati alipohojiwa na shirika la habari la IRNA kuhusu vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya taifa la Iran na kuongeza kuwa, siasa za rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu Iran si tu si jambo jipya lakini pia ni kujirudia kwa historia.

Liangxiang amezungumzia pia nafasi ya lobi ya Kizayuni katika maamuzi ya Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, lobi hiyo ya Kizayuni daima inazichochea serikali za Marekani na kuizuia Washington kuchukua msimamo wowote mzuri kuhusu Iran.

Viongozi wa Marekani wamehamakishwa mno na hatua ya walimwengu ya kupuuza vikwazo vya Washington dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 

 

Tarehe 8 Mei 2018, Donald Trump alitangaza kuitoa Marekani katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na vile vile aliamua kurejesha vikwazo ambavyo vilikuwa vimeondolewa dhidi ya Iran baada ya kufikiwa mapatano hayo. Marekani imetekeleza vikwazo vyake hivyo dhidi ya Iran kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilianza tarehe 7 Agosti na ya pili tarehe 5 Novemba mwaka huu.

Hata hivyo hatua hizo cha chuki za Trump dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinaendelea kulaaniwa kote ulimenguni hadi leo hii.

Tags

Maoni