Dec 14, 2018 04:34 UTC
  • Iran yajibu upayukaji wa waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, maneno ya kipuuzi na ya aibu ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni yanatokana na kuweweseka kwake kuhusu Iran, na kwamba kutoa vitisho vya kijeshi dhidi ya nchi kubwa kama Iran bila ya shaka yoyote hakuwezi kuachwa vivi hivi, bali kutafuatiliwa katika jumuiya na taasisi za kisheria na za kimataifa.

Bahram Qassemi alisema hayo jana kujibu uwewesekaji wa hivi karibuni kabisa wa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ambaye alisema hakanushi uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kijeshi ndani ya mipaka ya Iran na kuongeza kuwa, Iran ina nguvu kubwa za kiulinzi na kijeshi pamoja na uungaji mkono wa pande zote wa wananchi kiasi kwamba ndoto hizo zilizojaa chuki na za kupenda vita za Wazayuni kamwe hazitatimia bali zitawafanya wajute wale wanaoropoka matamshi kama hayo ya kigonjwa na ya watu waliochanganyikiwa. 

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akiungulika kwa chuki dhidi ya Iran na Waislamu

 

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umesimama juu ya msingi wa uvamizi na kutoa vitisho dhidi ya nchi za eneo hili na kusisitiza kuwa, Israel ndiyo inayoharibu zaidi utulivu na usalama na ndicho chanzo vya vita na mauaji ya kila namna katika eneo la Mashariki ya Kati lakini haioni hata aibu kujifanya kuwa ina wasiwasi na usalama wa eneo hili.

Vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran muda wote imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha usalama, utulivu na amani, ustawi na maendeleo katika eneo hili na daima itaendelea kuvunja njama za wasiolitakia kheri taifa na nchi hiii.

Tags

Maoni