Dec 16, 2018 07:48 UTC

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi yake vitashindwa tu na kamwe havitoweza kubadilisha siasa za Tehran.

"Hatuwezi kupinga kwamba sasa hivi tunakabiliwa na mashinikizo ya kiuchumi kutokana na vikwazo vya Marekani. Na hatupingi kuwa Marekani inaweza kusababisha matatizo kwa nchi nyingine. Lakini je, jambo hilo linaweza kubadilisha siasa za nchi? Nasema kwa kujiamini kwamba kamwe haliwezi," amesema Zarif wakati akihutubia Jukwaa la Doha la 2018 jana Jumamosi.

Doha Forum 2018

 

"Kama ni kipaji, basi kipaji cha kweli kiko nchini Iran na tunaweza kuwafunza wengine kipaji hicho kama zawadi, nacho ni kipaji cha kugeuza vikwazo kuwa fursa bora," amesema.

Ijapokuwa Marekani imeweka vikwazo vingi mno dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi cha miaka yote hii 40 ya tangu kuundwa dola la Kiislamu humu nchini, lakini imeshindwa kuifanya Tehran isalimu amri mbele ya ubeberu wa Marekani.

"Tumeweza kusimama imara kukabiliana njama za Marekani… kwa miaka 40 sasa, na ninaamini kwamba tunao uwezo wa kuendelea kukabiliana na Marekani kwa miaka mingine 40," amesema waziri huyoi wa mambo ya nje wa Iran.

Vile vile amesema, kama manufaa ya kitaifa ya Iran yatadhaminiwa kupitia mapatano ya nyuklia ya JCPOA na iwapo Umoja wa Ulaya utaheshimu vipengee vya mapatano hayo, bazi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nayo itaendelea kuyaheshimu.

Tags

Maoni