Dec 17, 2018 02:40 UTC
  • Ndege za Abiria za Iran Air zaendelea kuruka licha ya vikwazo vya Marekani

Ndege za Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran maarufu kama Iran Air zinaendelea kuruka katika anga za kimataifa pamoja na kuwepo vikwazo vya kidhalimu vya Marekani.

Bi. Farzanah Sharafbafi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo Jumapili alasiri pembizoni mwa Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Usafiri na Uchukuzi hapa Tehran. Ameongeza kuwa,  kwa miaka kadhaa sasa Iran imezoea kuwekwea vikwazo vya kidhalimu na Marekani lakini pamoja na kuwepo vikwazo hivyo, ndege za Shirika la Iran Air mbali na kuwa zinahudumu katika maeneo mbali mbali ya dunia zinafanyiwa ukarabati kamili pia ndani ya Iran.

Shirika la Ndege la Iran Air ndilo shirika la ndege ambalo limehudumu kwa muda mrefu zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na hivi sasa linafika katika maeneo 40 ndani na nje ya nchi.

Bi. Farzanah Sharafbafi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Maonyesho ya Tatu ya Kimataifa ya Usafiri na Uchukuzi ya Tehran yalianza Jumapili na yanatazamiwa kumalizika Jumanne. Lengo la maonyesho hayo ni kuonyesha mafanikio ya hivi karibuni ya kiteknolojia katika uga wa usafiri na uchukuzi nchini Iran.

Tags

Maoni