Feb 09, 2019 03:47 UTC
  • Satalaiti ya Iran ikiwa tayari kurushwa katika anga za mbali
    Satalaiti ya Iran ikiwa tayari kurushwa katika anga za mbali

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi yasiyo na msingi ya watawala wa Marekani kuhusu mpango wa Iran wa kurusha satalaiti katika anga za mbali na makombora na kusema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake ya kujihami.

Akizungumza na Shirika la Habari la ISNA  Ijumaa, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria madai ya wakuu wa Marekani kuwa eti mpango wa Iran wa makombora ni ukiukwaji wa Azimio 2231 la Baraza la Usalama na kusema madai hayo ni ya uongo na kungeza kuwa: "Shughuli za Iran katika sekta ya makombora hazikiuki hata kidogo azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa,  hatua ya Marekani kujiondoa kwa hamaki na bila mantiki katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ambayo yalikuwa ya kimataifa, imeplekea nchi hiyo itengwe na sasa inatoa madai dhidi ya Iran ili kujaribu kufunuika kosa lake la kistratijia.

Qassemi amesema uwezo wa makombora ya Iran ni sehemu ya uwezo halali wa kujihami na pia makombora hayo yanadhamini usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Qassemi amesema kwa kuzingatia uzoefu wa vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran, Wairani wataendelea kujiimarisha katika uga wa kijihami.

Kombora la Emad la Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemhutubu  Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani na kusema iwapo Pompeo amesahau, basi washauri wake vijana watamkumbusha namna wale waliokuwa wakitawala Marekani waliunga mkono utawala wa zamani wa Saddam nchini Iraq na kuuchochea kuanzisha vita vya miaka minane dhidi ya Iran.

Kwa upande wake Sergei Ryabkov Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia hivi karibuni alikosoa msimamo wa Marekani kuhusu mpango wa  Iran wa kurusha satalaiti anga za mbali na makombora na kusema, kwa kurusha satalaiti katika anga za mbali au kufanya majaribio ya makombora, Iran haikiuki sheria yoyote ya kimataifa.

Tags

Maoni