Feb 23, 2019 07:49 UTC
  • Yukiya Amano: Iran imefungamana kikamilifu na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, Iran imekuwa ikitekelezMkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA)a ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Yukiya Amano amesema hayo katika ripoti yake ya 14 kuhusiana na utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia ya mpango Kamili wa pamoja wa Utekelezaji JCPOA ambapo amethibitisha kwa mara nyingine tena kwamba, Tehran imefungamana kikamilifu na makubaliano hayo.

Sehemu moja ya ripoti yake hiyo aliyoitoa hapo jana, Yukiya Amano amesema kuwa, Iran imefungamana kikamilifu na suala la utekelezaji wa ahadi zake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema bayana kwamba, hakuna ishara zozote zinazoonyesha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekengeuka au kuhalifu ahadi zake kuhusiana na makubaliano hayo.

Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA)

Ripoti za mara kwa mara za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki zimekuwa zikisisitiza kuwa Iran imetekeleza na kuheshimu vipengee vyote vya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za kundi la 5+1. 

Itakumbukuwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka jana Rais wa Marekani, Donald Trump aliiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, suala ambalo limekumbwa na upinzani mkubwa wa nchi nyingine zilizofanikisha makubaliano hayo ya kimataifa.

Maoni