Mar 18, 2019 01:20 UTC
  • Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq: Marekani haina ruhusa ya kutumia ardhi ya Iraq dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq amesisitiza kuwa, Marekani haina ruhusu ya kuzichukulia hatua nchi jirani hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia ardhi ya Iraq.

Akizungumza na televisheni ya Press yenye makao yake mjini Tehran, Ahmad al Sahhaf ameashiria umuhimu wa mazungumzo ya Rais Hassan Rouhani wa Iran na viongozi wa Iraq na akasema: Mazungumzo hayo yatakuwa na taathira kubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili na ukaribu wa mataifa hayo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq ameashiria pia madai yanayotolewa na viongozi wa Marekani kwamba wanajeshi wa nchi hiyo wapo Iraq kwa ajili ya kufuatilia harakati za Iran katika eneo la Asia ya magharibi na kuongeza kuwa: Iraq haitatoa mwanya kwa yeyote yule kutumia ardhi yake kama kituo cha kuzisababishia madhara nchi jirani.  

Dr. Ahamd al Sahaf
 

Ahmad al Sahhaf ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi la Iraq vikishirikiana na makundi ya kujitolea ya wananchi vimeibuka na ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh baada ya miaka kadhaa ya mapambano, na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imefanya juhudi kubwa katika uwanja huo na hivi sasa iko tayari kushirikiana na jirani zake katika kipindi cha kuijenga upya nchi hiyo.   

Tags

Maoni