Mar 20, 2019 07:45 UTC
  • Iran yakanusha vikali madai ya kudukua simu za Wazayuni

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekanusha vikali madai ya utawala haramu wa Israel kwamba Tehran imedukua mawasiliano ya simu ya maafisa wa Kizayuni.

Bahram Qassemi aliyasema hayo jana Jumanne hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, maafisa wa Kizayuni wamezoea kusema urongo katika kila jambo, na kukuza mambo yasiyo na maana.

Amesema maafisa wa utawala bandia wa Israel wakishirikiana na wa Marekani wanafanya kila wawezalo kushadidisha mashinikizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu sambamba na kueneza chuki dhidi ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataja madai hayo ya Wazayuni kama njozi na ndoto za alinacha, yenye lengo la kuendeleza vita vya kisaikolojia dhidi ya taifa la Iran.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Qassemi amebainisha kuwa, "Iran inawategemea vijana wake waliobobea katika uga wa teknolojia katika kufanikisha masuala ya msingi na wala sio kufanya mambo ya kipuuzi kama udukuzi."

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa, mfumo wa itelijensia wa Iran umedukua mawasiliano ya simu ya aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Israel, Benny Gantz, ambaye ndiye mpinzani mkuu wa Waziri Mkuu wa utawala huo khabithi, Benjamin Netanyahu katika uchaguzi ujao wa bunge la Knesset.

 

 

Tags

Maoni