Apr 25, 2019 14:10 UTC
  • Iran yatoa onyo kwa Saudia na Bahrain zisimfuate kibubusa Trump

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa onyo kwa tawala za kiimla za Saudi Arabia na Bahrain zisimfuate kibubusa rais wa Marekani Donald Trump katika vikwazo vyake vya mafuta dhidi ya Iran na kuzitaka zifikirie matokeo mabaya ya hatua yao hiyo.

Sayyid Abbas Mousavi amesema hayo leo na kuongeza kuwa, serikali ya taifa la Iran hawawezi kusahau uadui wa baadhi ya nchi katika kipindi hiki cha kihistoria na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitoruhusu nchi yoyote ile kuchukua nafasi ya Iran katika soko la mafuta na kwamba lawama za matokeo yote mabaya ya uchokozi huo dhidi ya Tehran zitabebwa na Marekani na nchi vibaraka wake.

Siku ya Jumanne, tawala za kiimla na kiditeta za Saudi Arabia na Bahrain zilidai kuwa hatua ya rais wa Marekani ya kufuta ruhusa kwa baadhi ya nchi kununua mafuta ya Iran eti ni hatua nzuri na dharura kuchukuliwa.

Kadiri viongozi wa nchi za Kiarabu wanavyojikomba kwa Wamarekani ndivyo wanavyozidi kupoteza itibari yao

 

Siku hiyo ya Jumanne, Marekani iliendeleza hatua zake cha chuki dhidi ya Iran na kutangaza kuwa haitaongeza nguvu ruhusa kwa nchi zinazonunua mafuta ya Iran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia pia jinai ya Saudi Arabia ya kuwanyonga kwa umati watu 37 nchini humo na kusema kuwa kitendo hicho kinafanana na vitendo vya kikatili vilivyokuwa vinatendeka katika Bara Arabu kabla ya kuja dini tukufu ya Kiislamu.

Mousavi vile vile ameonya kwamba, Saudi Arabia ndiyo inayobeba lawama za jambo lolote baya linalotokea katika eneo hili kutokana na siasa zake za kueneza fitna zinazoungwa mkono na Marekani.

Tags

Maoni