Jul 26, 2016 04:24 UTC
  • Wazayuni watuhumiwa kuiba viungo vya miili ya Wapalestina

Jeshi la Israel limetajwa kuwa linaiba viungo vya Wapalestina na kufanya mauaji ya kizazi.

Mkutano uliofanyika nchini Ujerumani kujadili hali ya kijamii ya vijana wa Palestina umelituhumu jeshi la Israel kuwa linaiba viungo vya raia wa Palestina na kufanya mauaji ya kimbari huko katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. 

Mkutano huo pia umeonesha picha za mauaji ya kimbari na maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Palestina.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa Ujerumani ni manyanyaso na mateso wanayopewa raia wa Palestina wanaoshikiliwa katika jela za kutisha za Israel. 

Askari wa Israel wakimpeleka mtoto wa Palestina kusikojulikana

Hii si mara ya kwanza utawala haramu wa Israel kutuhumiwa kwamba unaiba viungo vya miili ya Wapalestina. 

Hivi karibuni pia Kituo cha Utafiti cha Jerusalem kiliripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeiba viungo vya Wapalestina 138 waliouawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Israel.   

Tags

Maoni