Aug 02, 2016 15:43 UTC
  • Spika wa bunge la Iraq azuiwa kutoka nje ya nchi

Waziri Mkuu wa Iraq amemzuia Spika wa bunge la nchi hiyo kutoka nje ya nchi.

Haidar al Abadi leo ametoa dikrii akimpiga marufuku Salim al Jabouri Spika wa bunge la nchi hiyo na wabunge wengine kadhaa kusafiri nje ya nchi baada ya Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Khalid al Obeidi kusema kuwa spika huyo amehusika katika utiaji saini mikataba ya silaha kinyume cha sheria. Waziri Mkuu wa Iraq amesema Spika wa bunge haruhusiwi kutoka nje ya nchi hadi itakapotolewa taarifa. 

Haidar al Abadi Waziri Mkuu wa Iraq 

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa watu wote ambao majina yao yametajwa katika sakata hilo la mikataba haramu ya  silaha,  hawapasi kutoka nje ya Iraq hadi uchunguzi utakapokamilika. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq imetangaza kuwa tayari tume imeundwa kuchunguza tuhuma hizo kwa kuzingatia kwamba tuhuma hizo zinazomkabili Spika wa bunge ni hatari. Waziri wa Ulinzi wa Iraq alimtuhumu Spika wa bunge la nchi hiyo kuwa amehusika na mikataba hiyo haramu ya silaha katika kikao cha hivi karibuni cha bunge hilo ambacho kiliitishwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye Waziri huyo wa Ulinzi. 

Tags

Maoni