• Hamid Karzai: Marekani ndio iliyoanzisha genge la kigaidi la Daesh

Rais wa zamani wa Afghanistan, Hamid Karzai amesema kuwa, Marekani ndiyo ilianzisha kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kwa ajili ya kufikia maslahi yake haramu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Karzai amesema, Marekani ndiyo muhusika mkuu wa kupatikana kwa kundi la kigaidi la Daesh na amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wake yeye, hakuna tofauti baina ya Marekani na kundi hilo la kigaidi.

Rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai 

Akizungumzia hatua ya Marekani ya kufyatua bomu la "Mama wa Mabomu Yote" lenye uzito wa tani 11 za mada za milipuko ya TNT na lenye uharibifu mkubwa zaidi kuliko mabomu yote yasiyo ya nyuklia duniani katika mji wa Achin mkoa wa Nangarhar amesema kuwa, lengo la Washington katika hatua hiyo haikuwa kuwapiga magaidi wa Daesh kama inavyodai, bali ilikuwa ikijaribu nguvu zake dhidi ya Russia.

Bomu lililopigwa na Marekani huko Afghanistan

Kadhalika rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai amezungumzia mahusiano yaliyopo baina ya kundi la kigaidi la Taleban na Marekani na kuongeza kuwa, hadi sasa Washington na kundi hilo huwa wanafanya mazungumzo.

Apr 21, 2017 16:56 UTC
Maoni