Hali ya kibinadamu inaripotiwa kuwa mbaya sana na ya kusikitisha, na miezi karibu 30 ya mashambulizi ya kila upande ya Saudi Arabia na washirika wake yanaonesha sura ya kutisha ya vifo vya maelfu ya watu wasio na hatia huku kile kinachoitwa jamii ya kimataifa ikiendelea kutazama kwa macho tu bila ya kuchukua hatua yoyote ya maana.

Kasi ya kueneza ujonjwa wa kipindupindu nchini Yemen sambamba na ukosefu wa huduma za awali kabisa za afya na tiba baada ya mashambulizi ya ndege za Saudi Arabia kuharibu kabisa hospitali na vituo vya afya vya nchi hiyo, imesababisha hali isiyoelezeka kwa maneno na sasa kipindupindu kimekuwa silaha hatari ya mauaji ya Waislamu wa Yemen sambamba na silaha za kisasa na zile zilizopigwa marufuku zinazotumiwa na Saudia na washirika wake katika vita vya Yemen. Kuhusu kasi ya maambukizi ya kipindupindu, televisheni ya al Alam imeripoti kuwa: Wagonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya Yemen wanarandaranda huko na kule wakitafuta tiba bila ya mafanikio, na kwamba maji machafu na taka zilizosambaa katika magofu ya nyumba zilizoharibiwa na mashambulizi ya Saudia na washirika wake vinazidisha kasi ya kuenea ugonjwa huyo. Ripoti hiyo inasema, visima na mabwawa ya maji pia yameambukizwa kwa makusudi bakteria wa kipindupindu. 

Wayemen wanaangamizwa kwa kipindupindu

Tamwimu zinaonesha kuwa, Myemeni mmoja kati ya kila 120 wanaopatwa na ugonjwa wa kipundupindu kila siku anapoteza maisha na kwamba karibu Wayemeni 2,000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo tangu mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. Vilevile Wayemeni laki nne wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu. Kasi ya kuenea ugonjwa huo na mapana yake inaonesha kuwa, ugonjwa huo ni sera na silaha inayotumiwa kwa ajili ya kutimiza malengo na mipango ya Saudia katika nchi hiyo. Hivi karibuni tovuti ya habari cha Transcend Media Service (TMS) ilichapisha ripoti ya kutisha kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na Saudi Arabia na Marekani kwa mpangilio maalumu huko Yemen na kuandika kuwa: Ugonjwa wa kipindupindu umeenea kwa kiwango kikubwa sana nchini Yemen na vyanzo vya maji na mfumo wa majitaka wa nchi hiyo vimeharibiwa kabisa kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia. Ripoti ya Transcend Media Service (TMS) imeendelea kusema: "Hali hiyo imepeleka kuchafuka kwa maji ya matumizi ya binadamu kwa bakteria hatari wa Vibrio cholerae wanaosababisha ugonjwa wa kipindupindu ambayo sasa watumiwa na Marekani na Saudi Arabia kama silaha ya kuwaua watu wa Yemen". 

Watoto wadogo anakufa kila siku kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na kukosa huduma za afya

Jambo linalodhihirishwa na hali ya sasa inayotokana na kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu, kudumishwa mzingiro wa Wayemeni, na kubwa zaidi, kufungwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana'a ni siasa zenye malengo maalumu za wavamizi wa Kisaudia na Marekani za mauaji ya umati dhidi ya watu wa Yemen. Vilevile upuuzaji wa jamii ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kuhusu maafa hayo ya kibinadamu una maana ya kushirikiana na makatili na wauaji hao wanaoangamiza kizazi cha Yemen na hawaoni ajizi au soni na haya kutumia silaha za biolojia kama bakteria wa Vibrio cholerae kwa ajili ya kuua watu wasio na hatia yoyote wa Yemen.

Wauaji wa taifa la Yemen

Maafa hayo yanakuwa makubwa zaidi pale Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric anaposimama mbele ya waandishi wa habari na kuisema, umoja huo hauna masulia na majukumu yoyote kuhusu uwanja wa ndege wa Sana'a!! Hii ni kwa sababu, kufungwa uwanja huo mbali na kwamba, kunazidisha mara dufu mgogoro wa usalama wa chakula, madawa na kadhalika nchini Yemen, vilevile kunakamilisha mradi wa kueneza zaidi ugonjwa wa kipindupindu nchini umo. Hatua ya Saudi Arabia ya kufunga uwanja huo pia inazuia kupelekwa nje ya nchi wagonjwa wanaohitaji huduma ya matibabu katika nchi za nje. Duru za Yemen zinaripoti kuwa, zaidi ya raia elfu 13 wa nchi hiyo wamefariki dunia kutokana na kushindwa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu au kutokana na ukosefu wa dawa walizohitajia.

Aug 13, 2017 02:17 UTC
Maoni