• Mrithi wa Ufalme wa Saudia alifanya safari ya siri Israel

Tovuti moja ya habari ya Kizayuni imeripoti kuwa Muhammad bin Salman, mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia wiki iliyopita alifanya safari ya siri huko Tel Aviv ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu.

Tovuti ya habari ya IUVMONLINE imeripoti kuwa afisa mmoja wa intelijinsia wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amethibitisha kufanyika safari hiyo na kueleza kwamba Anwar Ashqi, jenerali mstaafu na mtu aliye karibu na ukoo unaotawala Saudi Arabia wa Aal Saud pamoja shakhsia wengine kadhaa wa ngazi za juu wa nchi hiyo waliandamana na Muhammad bin Salman katika safari hiyo.

Afisa huyo wa Imarati ambaye ametaka jina lake lisitajwe ameongeza kuwa Wasaudi wanataka kuimarisha uhusiano na Israel katika muelekeo wa kuutambua rasmi utawala huo ili iwe rahisi kwa Riyadh kupata mikopo kwa Mfuko wa Kimataifa wa Fedha (IMF) na Benki ya Dunia.

Redio ya Sauti ya Israel nayo pia imeashiria maudhui ya safari iliyofanywa na ujumbe wa nchi moja ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi huko Tel Aviv lakini ofisi ya Netanyahu na Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni zimekataa kueleza chochote kuhusu suala hilo.Hii ni katika hali ambayo siku chache zilizopita Waziri Mkuu huyo wa utawala haramu wa Kizayuni alisema kuwa uhusiano wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu umefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Kuwa bega kwa bega Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel katika kutekeleza siasa za kupiga vita muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati kwa madhumuni ya kudhoofisha muqawama na mapambano ya Wapalestina na kushirikiana tawala mbili hizo katika kuyaunga mkono makundi ya kigaidi katika eneo vimezidi kuweka wazi sura halisi ya tawala za Kizayuni na Aal Saud ambazo ni chimbuko la ugaidi.../

Sep 12, 2017 04:39 UTC
Maoni