• Ansarullah ya Yemen: Muungano wa Marekani unaunga mkono ugaidi

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani na unaojulikana kama wa kupambana na ugaidi jina lake linapaswa kuwa "Muungano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Ugaidi."

Abdul-Malik Badreddin al-Houthi amesisitiza kuwa, muungano huo umekuwa ukiunga mkono ugaidi badala ya kupambana nao.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Saudi Arabia haitasalimika na kugawika na kujitenga na kuongeza kwamba, mgawanyiko na mpasuko nchini Saudia utakuwa mkubwa zaidi kwani utawala huo ni wa kidikteta.

Aidha Abdul-Malik Badreddin al-Houthi amesema kuwa, Saudi Arabia imekuwa ikifanya juhudi za kutwisha satua na ushawishi wake ndani ya Yemen kwa kuwapuuza washirika wake.

Uharibifu unaofanywa na hujuma ya kijeshi ya Saudia na washirika wake dhidi ya Yemen

Kiongozi huyo wa Harakati ya Wananchi wa Yemen ya Ansarullah ameeleza kuwa, wako tayari kuzisaidia harakati huru nchini Saudia ili ziendeshe mapambano dhidi ya siasa zisizo sahihi zinazotekelezwa na utawala wa Aal Saud.

Abdul-Malik Badreddin al-Houthi ameashiria ushindi uliopatikana dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Syria, Iraq na Lebanon na kubainisha kwamba, ushindi wa nchi hizo dhidi ya magaidi wa Daesh ni ushindi wa Umma wote wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesaema kuwa, Saudia na Imarati zimekuwa na nafasi haribifu na zimekuwa zikifuatilia suala la kugawanyika eneo la Mashariki ya Kati, lakini makabila ya Yemen yako pamoja na bega kwa bega na wananchi wa Yemen katika kukabiliana na uvamizi wa Saudia dhidi ya nchi yao.

 

Oct 13, 2017 04:25 UTC
Maoni