• Sudan yapinga misimamo dhidi ya Iran ya baadhi ya nchi za Kiarabu

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa nchi yake haikubaliani na misimo iliyodhidi ya Iran na tangazo la vita la baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya Jamhuri ya Kislamu.

Omar al Bashir amesema kuwa, uhusiano na ujirani mwema baina ya nchi za Kiarabu na Iran hauwezi kupatikana kwa kutumia njia za kijeshi bali kwa mazungumzo.

Rais wa Sudan ameongeza kuwa, mpambano baina ya nchi za Kiarabu na Iran si hatua ya busara na utakuwa na madhara kwa eneo na kanda nzima ya Mashariki ya Kati. 

Rais Omar al Bashir wa Sudan alikuwa akiashiria kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kilichofanyika Jumapili iliyopita mjini Cairo nchini Misri kwa mwito wa Saudi Arabia kujadili maudhui ya Iran. 

Kikao hicho kilichosusiwa na nchi za Qatar, Lebanon, Iraq, Syria, Oman na Algeria kilitawaliwa na madai ya kukaririwa na yasiyo na msingi ya serikali ya Riyadh dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na harakati ya Hizbullah ya Lebanon. 

Ibrahim Ghandour

Jumanne iliyopita pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ibrahim Ghandour alisema kuwa, Khartoum kamwe haitajiunga na muungano wa Saudi Arabia kwa ajili ya kukabiliana na Iran.

Tags

Nov 23, 2017 03:27 UTC
Maoni