• Israel: Vita vijavyo kati yetu na HAMAS vitatudhoofisha kwa ndani

Waziri wa Makazi wa Utawala Haramu wa Israel, Yoav Galant amesema kuwa uwezo wa shabaha wa makombora ya Brigedi ya Izzudeen Qassam tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, utaidhoofisha Israel kwa ndani.

Kanali ya Namba ya Pili ya televisheni ya utawala huo wa Kizayuni sambamba na kutangaza suala hilo kwa kumnukuu Galant, imeonyesha pia uwepo wa tofauti kali kati ya baraza la mawaziri la Israel juu ya namna ya kukabiliana na Ukanda wa Gaza.

Moja ya makombora ya muqawama wa Palestina HAMAS

Kwa mujibu wa televisheni hiyo, baadhi ya mawaziri wa utawala huo khabithi wameonya kwamba, kuendelea matatizo ya kiuchumi katika eneo la Gaza kunaweza kuibua vita vipya na Israel na kwamba Tel Aviv haipo tayari kuingia katika vita hivyo. Uwezo wa makombora ya muqawama wa Palestina umeendelea kuongezeka siku hadi siku, licha ya eneo la Gaza kuwekewa mzingiro wa kila upande kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Eneo hilo linazingirwa ardhini, angani na baharini tangu mwaka 2006, huku Israel ikizuia kutumwa eneo hilo hata bidhaa muhimu za msingi kama vile chakula, madawa na nishati.

Yoav Galant, Waziri wa Makazi wa Utawala Haramu wa Israel

Pamoja na hayo utawala wa Kizayuni ambao kila siku umekuwa ukipatwa na tumbojoto juu ya mafanikio hayo ya Wapalestina umeshindwa kuzuia kuimarika uwezo wa muqawama wa Palestina.

Tags

Jan 02, 2018 07:32 UTC
Maoni