• Kuongezeka pakubwa vitendo vya kujiua miongoni mwa wanajeshi wa Kizayuni

Idadi ya wanajeshi wa Israel wanaojiua inazidi kuongezeka pakubwa kutokana na kulazimishwa kujiunga jeshini na kushindwa mtawalia utawala wa Kizayuni mbele ya muqawama wa Wapalestina.

Takwimu mpya zilizotolewa na ofisi ya msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni zinaonyesha kuwa wanajeshi 16 walijiua mwaka jana wa 2017; iadi ambayo imetajwa kuwa ni kubwa sana kulinganisha na mwaka 2011. Mirage Kirchner Kamanda wa Idara ya Nguvu Kazi katika jeshi la Kizayuni ametangaza kuwa mengi ya matukio ya kujiua yametokana na kulazimishwa wanajeshi wa utawala huo kujiunga jeshini.  

Wanajeshi wa Israel ambao wamechanganyikiwa kutokana na wengi wao kuendelea kujiua

Takwimu za hivi karibu zinaonyesha kuwa, mwaka jana wa 2017 jumla ya wanajeshi 55 wa Kizayuni waliuawa; kiwango ambacho kinatajwa kuongezeka ikilinganishwa na wanajeshi 41 waliojiua mwaka juzi wa 2016.  Jeshi la utawala wa Kizayuni liliainisha kundi la washauri na wataalamu wa masuala ya elimu jamii ili kutoa ushauri nasaha kwa wanajeshi wake katika vikosi mbalimbali vya jeshi la utawala huo hata hivyo zoezi hilo halikuwa na taathira yoyote. Wanajeshi wa Israel wanaona kuwa njia pekee ya kukwepa kushiriki vitani ni kuamua kujiua.  

Tags

Jan 03, 2018 07:53 UTC
Maoni