Jan 06, 2018 16:49 UTC
  • Hizbullah: Kuvunjiwa heshima Quds ni matunda ya mchezo wa kudansi na upanga wa Trump na Salman

Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Nabil Qaouk amezitaja siasa za Saudia kuwa za maafa na kuongeza kuwa, kitendo cha kuvunjiwa heshima mji wa Quds na msikiti wake kinatokana na mchezo wa kudansi na upanga wa Rais Donald Trump wa Marekani na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudia.

Sheikh Nabil Qaouk ameyasema hayo katika marasimu yaliyofanyika eneo la al-Ghamiq mjini Beirut na kusema kuwa, hivi sasa Saudia imebadilika na kuwa muibua fitina katika eneo la Mashariki ya Kati na kwamba watawala wa nchi hiyo wamekuwa wakiwapokea na kuwakumbatia maadui wa umma wa Kiislamu sambamba na kuwatunuku zawadi ya mamilioni ya dola na kufunga nao mikataba ya mamia ya mamilioni ya dola. 

Sheikh Nabil Qaouk

Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amefafanua kuwa, lau kama Saudia isingewaita makumi ya wanawafalme na viongozi wengi wa Kiarabu na Kiislamu kwenda Riyadh kutoa baia kwa Rais Donald Trump wa Marekani, wakati rais huyo alipofanya ziara nchini Saudia, Washington isingethubutu kuvunjia heshima au kucheza na matukufu ya umma wa Kiislamu na Kiarabu.

Mfalme Salman wa Saudia akimvisha mkufu wa dhahabu Trump

Kadhalika Sheikh Nabil Qaouk amesisitiza kuwa kosa kubwa la utawala wa Saudia lilikuwa ni kumfungulia mlango Trump kwenye siasa za uhasama dhidi ya umma wa Kiislamu na kwamba kosa kubwa la umma wa Kiislamu ni kuitelekeza al-Quds na kumruhusu rais huyo wa Marekani kuendesha harakati zake sambamba na kupanga njama usiku na mchana dhidi ya Iran na muqawama.

Tags

Maoni