• Atallah Hanna, Askofu Mkuu wa kanisa la Orthodox Catholic Church la Palestina
    Atallah Hanna, Askofu Mkuu wa kanisa la Orthodox Catholic Church la Palestina

Askofu Mkuu wa Kanisa la Rome Orthodox linalojulikana kwa jina rasmi la Orthodox Catholic Church katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, kwa mara nyingine tena amelaani jinai za Israel dhidi ya Wakristo na Waislamu na kusema kuwa, mji wa Quds (Yerusalemu) ni mali ya Wapalestina si mji wa Wazayuni.

Televisheni ya al Mayadeen ya nchini Lebanon imemnukuu Askofu Mkuu Atallah Hanna akisema hayo na kusisitiza kuwa, wananchi wote wa Palestina, wawe Waislamu au Wakrsto, wataendelea kusimama kidete kuutetea mji mtakatifu wa Yerusalemu (Quds).

Kanisa la Miracle lililochomwa moto na Wazayuni wenye chuki za kidini huko Palestina

 

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Mashariki huko Palestina pia amesema, kanisa la East Orthodox Church litaendelea kuungana na Wapalestina wengine kukabiliana na siasa za rais wa Marekani, Donal Trump na Wazayuni wavamizi pamoja na njama zote zilizo dhidi ya Yerusalemu (Quds) na zinazokwenda kinyume na malengo matakatifu ya Palestina. Askofu Hanna ameongeza kuwa: Yerusalemu (Quds) ni mali ya wananchi wa Palestina na kwamba mateka wa Kipalestina walioko katika makucha ya Wazayuni ni wana wa ardhi hiyo, hivyo ni lazima kuwaunga mkono.

Tangu tarehe 6 Disemba 2017, ardhi za Palestina zimekuwa uwanja wa maandamano makubwa na malalamiko ya kila upande ya kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa uamuzi wake wa kuitangaza Quds kuwa eti mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel. Baadhi ya viongozi wa Kikristo ndani na nje ya Palestina wameungana na wapenda haki na amani duniani kulaani kitendo hicho cha kibeberu cha rais wa Marekani.

Wakristo wakiandamana kuilaani Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni

 

Hadi hivi sasa Wapalestina 21 wameshauawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika maandamano yanayoendelea huko Palestina. Zaidi ya Wapalestina 500 wametekwa nyara na wanajeshi katili wa Israel tangu Trump alipotangaza kuwa Quds eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Tags

Jan 13, 2018 07:49 UTC
Maoni