Feb 09, 2018 07:56 UTC
  • Al Wifaq ya Bahrain: Tutaendelea na mapinduzi hadi kuung'oa utawala Aal Khalifa

Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq ya Bahrain imetangaza kuwa, itaendeleza mapambano yaliyoanza Februari 14 mwaka 2011 kwa lengo la kuuondoa madarakani utawala wa Aal Khalifa.

Jumuiya ya al Wifaq imesisitiza kuwa itaendelea na mapinduzi yake ya Februari 14 chini ya nara za "Bado tupo hadi kupinduliwa utawala ulioko madarakani" na kuongeza kuwa, nara hiyo inadhihirisha istiqama na kuwa tayari wananchi wa Bahrain  kwa ajili ya mabadiliko na mageuzi' ambapo mara hii wataingia uwanjani kwa irada thabiti zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. 

Taasisi hiyo ya Kiislamu ya Bahrain imeashiria udharura wa kuendelezwa maandamano ya amani dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo na kueleza kuwa, kufikiwa mapatano ya kitaifa ni njia pekee inayoweza kuiondoa Bahrain katika mgogoro wa sasa kwa sababu miaka saba ya subira na istiqama imethiibitisha kwamba migogoro haiwezi kupatiwa ufumbuzi kwa njia za mabavu. 

Wananchi wa Bahrain wamekuwa na subira mbele ya ukandamizaji wa askari wa Bahrain  

 

Makundi ya kimapinduzi ya Bahrain yanayoyajumisha Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya Februari 14, Jumuiya ya Kiislamu ya al Wifaq, Harakati ya Haki, Mrengo wa Harakati ya Kiislamu na Harakati ya Uokovu zimechagua shaari ya "Bado Tupo Hadi Kupinduliwa Utawala Ulioko Madarakani" ili kushirikiana katika maadhimisho ya mwaka wa saba tangu kuanza harakati ya mapinduzi ya wananchi wa Bahrain mwezi Februari mwaka 2011. Makundi hayo ya kimapinduzi ya Bahrain yameyatolewa wito matabaka mbalimbali ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya kuanza vuguvugu la mapinduzi nchini humo. 

Tags

Maoni