• Wimbi la pili la maandamano ya wananchi nchini Bahrain laanza kwa mnasaba wa Februari 14

Wimbi la pili la maandamano na harakati ya malalamiko ya wananchi nchini Bahrain kwa mnasaba wa mwaka wa saba wa mapinduzi ya tarehe 14 Februari, limeanza jioni ya leo Jumatano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Katika wimbi hilo jipya la maandamano, washiriki wamechoma moto matairi na kuzusha moshi mzito kama ishara ya kuanza kwa harakati hiyo ya maandamano katika mitaa mbalimbali ya Bahrain sambamba na kufunga njia. Sambamba na kuanza kwa maandamano hayo, askari wa utawala wa Aal Khalifa wamewashambulia waandamanaji katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ambapo katika kujaribu kuwatawanya wametumia gesi ya kutoa machozi na silaha za moto.

Askari wa utawala wa Aal Khalifa wakitumia mabavu dhidi ya raia wa kawaida

Inafaa kuashiria kuwa, tarehe 14 Februari inakkumbushia kuanza mapinduzi ya amani ya wananchi nchini Bahrain. Ni miaka saba sasa imepita tangu wananchi wa nchi hiyio walipoanzisha maandamano ya amani wakilalamikia kufanyika mabadiliko muhimu ya kkisiasa. Hata hivyo badala ya utawala wa Aal Khalifa kusikiliza malalamiko ya wananchi ulitumia ukandamizaji wa kuchupa mipaka sambamba na kuomba masaada zaidi wa askari vamizi wa Saudia walioingia nchini humo na kufanya jinai nyingi dhidi ya binaadamu.

Hali ya sasa nchini Bahrain

Utawala wa Aal Khalifa kwa kushirikiana na Aal Saud mbali na kufanya mauaji na jinai mbalimbali dhidi ya waandamanaji, uliwatia pia mbaroni mamia ya wanaharakati wa kisiasa huku ukiwahukumu vifungo vya kidhalimu ikiwemo adhabu za kifo.

Tags

Feb 14, 2018 16:49 UTC
Maoni