• Jeshi la Yemen lafanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Saudia na kuua wanajeshi kadhaa

Wanajeshi kadhaa wa Saudia wameuawa baada ya jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi ndani ya ardhi ya Saudi Arabia.

Televisheni ya al Masira imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, mashambulizi hayo yamefanyika dhidi ya maeneo ya kijeshi ya Saudi Arabia katika eneo la Qais huko Jizan kusini mwa Saudia na mbalimbali na kuua wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia, yameteketeza pia magari kadhaa ya wanajeshi wa utawala wa ukoo wa Aal Saud.

Jeshi la Yemen limefanikiwa kuwatia nguvuni pia mamluki wanne wa Saudia katika mapigano hayo. 

Wasaudia katika maziko ya wanajeshi wao

 

Duru nyingine za habari za Yemen zimetangaza habari ya kuuawa wanajeshi kadhaa wa Saudi Arabia katika maeneo ya Jazan na Najran, kusini mwa Saudia. Taarifa zinasema kuwa watunguaji stadi wa jeshi la Yemen na harakati ya Answarullah wamefanya mashambulizi makali katika maeneo ya mpakani mwa Yemen na Saudi Arabia.

Siku ya Jumatatu, watunguaji hao stadi wa jeshi la Yemen walimpiga risasi na kumuua mwanajeshi mmoja wa Saudia katika kambi ya kijeshi la al Haskul huko Jazan, kusini mwa Saudia. Operesheni za watunguaji stadi wa jeshi la Yemen zimeongezeka sana tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018 na hadi sasa wamefanikiwa kuaa makumi ya wanajeshi wa Saudi Arabia.

Mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi ya jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi yamekuja kutokana na Saudi Arabia kufanya jinai zisizo na kikomo dhidi ya wananchi wa Yemen na kuharibu kila kitu katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu. 

Jizan, kusini mwa Saudi Arabia

 

Mar 07, 2018 07:33 UTC
Maoni