• Safari ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia nchini Uingereza, Silaha Mkabala wa Kuunga Mkono Jinai

Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia, Mohammad Bin Salman, Jumatano aliwasili nchini Uingereza baada ya safari hiyo kuakhirishwa mara kadhaa.

Bin Salman alikuwa amepangiwa kutembelea Uingereza katika mwezi wa Januari lakini safari hiyo iliakhirishwa mara kadhaa kufuatia maandamano na malalamiko ya wananchi ambao walikuwa wanamkata Waziri Mkuu Theresa May asikutane na mrithi huyo wa ufalme wa Saudia.

Bin Salman amewasili London katika hali ambayo waliowengi nchini humo wanapinga safari yake hiyo jambo ambalo limelazimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al Jubeir aombe wapinzani wasitishe maandamano yao. Hakuna shaka kuwa, sababu ya upizani mkali wa safari ya Bin Salman mjini London inahusiana na jinai zisizo na kikomo za Saudia katika nchi jirani ya Yemen. Katika kipindi cha wiki mbili zijazo, utatimia mwaka wa nne tokea Saudia na waitifaki wake waanzishe vita vikubwa dhidi ya Yemen, nchini masikini zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Moja kati ya matokeo ya vita hivyo ni maafa makubwa ya kibinadamu nchini humo ambalo wati zaidi ya 14,000 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Aidha mamilioni wamelazimika kuwa wakimbizi huku mamilioni ya wengine nao wakiwa wanakabiliwa na njaa. La kusikitisha zaidi wanawake, watoto na wazee ndio waathirika wakuu wa vita hivyo ambavyo pia vimeharibu kabisa miundo msingi ya nchi hiyo kama vile mahospitali, shule, madaraja na misikiti. Jinai hizo za kivita za Saudia dhidi ya Wayemen zimelaaniwa kote duniani.

Watoto ni waathirika wa vita vya Saudia dhidi ya Yemen

Kile kinachotekelezwa na utawala wa Aal Saudi nchini Yemen ni jinai ya wazi ya kivita, jinai dhidi ya binadamu na jinai dhidi ya amani. Hizi ni jinai ambazo zimetajwa katika hati za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Kwa msingi huo, idadi kubwa ya watu wa Uingereza, shakhsia na taasisi za kirai nchini humo katika miezi ya hivi karibuni zimekuwa zikiandaa maandamano na kampeni ya kutaka kufutwa safari ya Mohammad bin Salman nchini humo na hata kusisitiza kuwa safari hiyo inamaanisha kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza anaunga mkono jinai za Saudia.

Gazeti la Independene la London limeandika hivi kuhusu kadhia hii: "Saudi Arabia inaeneza masaibu na adhabu katika nchi nyingine. Uingiliaji wa Saudia kijeshi katika vita vya Yemen kumepelekea kuuawa maelfu ya watu na kuibuka baa la njaa nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Amnesty International, ndege za kivita za Saudia zinalenga kwa makusudi raia na maeneo ya kiraia kama vile mahospitali, shule, masoko na misikiti nchini Yemen. Tokea mwanzo  wa vita vya Yemen, Mohammad bin Salman amekuwa akiongeza na kusimamia vita hivyo tokea siku ya kwanza."

Theresa May, Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye alilazimika kuahirisha safari ya Bin Salman kutokana na upinzani mkubwa, hatimaye amekaribisha mtawala huyo wa Saudia.

Kilicho wazi ni kwamba, May hataki Uingereza ikose faida kubwa ipatikanayo katika kuizuia Saudia silaha na kimsingi hataki nchi yake iachwe mbali na Marekani katika kuwauzia silaha watawala wa Riyadh. Katika safari yake nchini Saudia mwezi Mei mwaka 2017, Rais Donald Trump wa Marekani lifanikiwa kuishawishi Saudia itie saini mikataba yenye tahamni ya dola bilioni 400 ambapo dola 110 ni za ununuzi wa silaha.

Hivi sasa inaelekea kuwa safari ya Bin Salman Uingereza pia kwa kiasi kikubwa itajikita katika ununuzi wa silaha a Uingereza. Hivyo kama ambavyo Trump alisema Saudia ni kama ng'ombe wa Marekani wa kukamua maziwa, Uingereza pia ina mtazamo huo huo kuhusu Saudia. 

Saudia inalenga maeneo ya raia katika vita dhidi ya Yemen

Ni kwa msingi huo ndio Caroline Patricia Lucas mbunge wa chama cha kijani katika Bunge la Uingereza akaandika makala katika gazeti la Independent na kusema: "Inaelekea kuwa katika safari ya Bin Salman mjini London mikataba yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 100 itatiwa saini."

Uingereza imekuwa ikiuzuia Saudia zana za kivita zenye kugharimu mabilioni ya dola lakini pamoja na hayo Theresa May anataka Saudia inunue silaha zaidi. Hapana shaka kuwa akiwa London, Bin Salman atatia saini mikataba ya kununua silaha mpya zaidi za kutekeelza jinai za kivita na kuwakandamiza Wasaudi.

Nukta ya mwisho hapa ni kuwa, Uingereza haijali ni nani anatawala Saudia, awe ni Mohammad bin Salman au mwanamfalme mwingine yeyote, kilicho muhimu kwa Uingereza sawa na Marekani ni faida zinazopatikana na masuala kama demokrasia na haki za binadamu hayana maana hapa. Bin Salman kimsingi anatumia mabilioni ya dola za utajiri wa mafuta ya nchi hiyo 'kununua' uungaji mkono wa madola ya Magharibi na hivyo inapata uungaji mkono wa Uingereza katika jinai zake ndani ya Saudia na pia nchini Yemen.

Tags

Mar 08, 2018 01:37 UTC
Maoni