• Rais wa Ufaransa ampinga Trump, ataka Beitul-Muqaddas itambuliwe kuwa mji mkuu wa Palestina

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa, umewadia wakati sasa wa Beitul-Muqaddas kutambuliwa kuwa mji mkuu wa Palestina.

Rais wa Ufaransa ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, anaupinga uamuzi wa Rais wa marekani Donald Trump wa kuutambua mji wqa Beituil-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais wa Ufaransa amesisitiza kwamba, uamuzi huo wa Donald Trump haukubaliki na kwamba, utawadia wakati pia kwa mji wa Beitul Muqaddas kutambuliwa na waklimwengu kuwa mji mkuu wa Palestina.

Rais Emmanuel Macron amesisitiza kwamba, hatua ya upande mmoja ya Rais wa Marekani ya kuitambua Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa wa Israel hausadii chochote katika kuhitimisha mzozo uliopo.

Rais Donald Trump wa Marekani

Tarehe 6 Disemba mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani alichukua hatua ambayo nikinyume na maazimio ya kimataifa kwa kuitangaza Quds Tukufu (Jerusalem) kuwa ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel. Aidha alitangaza kuwa Marekani imeanzisha mchakato wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji huo kutoka Tel Aviv.

Ufaransa ni miongoni mwa nchi 13 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zilizopiga kura ya ndio kuunga mkono muswada uliowasilishwa na Misri uliokuwa ukitaka kubatishwa uamuzi huo wa Marekani.

Hivi karibuni Marekani ilitangaza kuwa, tarehe 14 Mei mwaka huu inayosadifiana na siku ya kukaliwa kwa mabavu Palestina, itafungua ubalozi wake huko Beitul-Muqaddas.

Tags

Mar 08, 2018 04:33 UTC
Maoni