• Shambulio la ndege za kivita za Saudia laua watu 6 wa familia moja mjini Sana'a, Yemen

Watu sita wa familia moja wameuliwa katika shambulio lililofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Raia wengine wawili wa Yemen wameuawa pia na wengine wanne wamejeruhiwa wakati ndege za kivita za utawala vamizi wa Aal Saud zilipofanya mashambulio katika mkoa wa Al Hudaydah magharibi mwa Yemen.

Katika jibu lao kwa hujuma hizo, vikosi vya Yemen vimeshambulia magari mawili ya kijeshi ya mamluki wa Saudia katika mji wa Al Jawf kaskazini mwa Yemen na kuwaangamiza wote waliokuwemo ndani yake.

Vikosi vya Yemen aidha vimefanikiwa kumwangamiza afisa mmoja wa kitengo cha jeshi la Saudia katika eneo la Sarwah, mkoani Ma'rib.

Mashambulio ya anga ya ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Yemen yangali yanaendelea huku yakibarikiwa na kimya cha jumuiya za kimataifa. 

Tangu mwezi Machi mwaka 2015, na kwa msaada na uungaji mkono wa Marekani, Saudia inaendelea kuishambulia kijeshi Yemen, ambapo hadi sasa imeshaua na kujeruhi makumi ya maelfu ya watu na kuwafanya mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Sehemu ya jinai za kinyama zinazofanywa na Saudia dhidi ya watoto wasio na hatia wa Yemen

Wakati huohuo Wizara ya Haki za Binadamu ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen imetangaza kupitia taarifa kwamba: zaidi ya wanawake na watoto 10,300 wameuawa na kujeruhiwa tangu ulipoanza uvamizi na mashambulio ya kijeshi ya Saudia na waitifaki wake.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa hadi sasa watoto laki mbili na 74 elfu kati ya watoto na wanawake milioni mbili na laki tano wanaokabiliwa na lisheduni wamefariki dunia kutokana taathira za mzingiro iliowekewa nchi hiyo na utawala wa Aal Saud.../

Mar 08, 2018 16:22 UTC
Maoni