Mei 20, 2018 02:22 UTC
  • Saudia yaanza duru mpya ya kuwakamata wale wanaopinga nchi hiyo kuwa  na uhusiano na Israel

Vyombo vya habari, wanasheria na wanaharakati mbalimbali wameelezea kupitia mitandao ya kijamii juu ya kuanza duru mpya ya kamatakamata ya utawala wa kifalme wa Aal-Saud dhidi ya wapinzani wanaopinga nchi hiyo kuwa na uhusiano na utawala katili wa Kizayuni.

Watawala wa Kiarabu hususan Aal-Saud wanafanya kila njama za kuboresha zaidi uhusiano na utawala haramu wa Israel unaokalia kwa mabavu kibla cha kwanza cha Waislamu, kwa kudhani kwamba kwa kufanya hivyo wataendelea kusalia madarakani kwa kupata uungaji mkono wa nchi za Magharibi hususan Marekani.

Gazeti la Al-Quds Al-Arabi ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kufichua ukandamizaji wa Saudia

Gazeti la Al-Quds Al-Arabi limewanukuu wanaharakati mbalimbali katika mitandao ya kijami, wakisema kuwa viongozi wa Saudia wamewatia mbaroni shakhsia kadhaa wakiwemo wanawake na wanaume wanaoendesha kampeni ya kupinga nchi hiyo kuwa na uhusiano na Israel. Kwa mujibu wa taarifa hiyo miongoni mwa wanaharakati waliotiwa mbaroni ni pamoja na Muhammad al-Rabia, Ibrahim Mudaimigh na Nura Faqiha. Wakati huo huo, Abdullah al-Ghamdi, mwanaharakati wa Saudia anayeishi nchini Uingereza amesema kuwa, viongozi wa Saudia wanawashikilia mama na kaka yake kwa zaidi ya siku 50 sasa huku wakikataa mtu yeyote kuwaona. Ghamdi anafahamika kwa kuendesha kampeni kubwa katika mitandao ya kijamii dhidi ya utawala wa kifalme wa Saudia na kupinga nchi hiyo kuboresha uhusiano wake na Tel Aviv.

Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International

Januari mwaka huu Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International sambamba na kuthibitisha habari ya kuhukumiwa wanaharakati wawili wa haki za binaadamu nchini Saudia ikiwa ni katika kuendelea kwa siasa za ukandamizaji za Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa nchi hiyo, lilionyesha wasi wasi wake kutokana na mwenendo huo wa kujaribu kukandamizwa sauti za malalamiko ya wananchi wa Saudiai.

Tags

Maoni