Mei 21, 2018 14:22 UTC
  • Silaha za magaidi zilizoundwa katika nchi wanachama wa Nato zanaswa Syria

Vyombo vya habari vya Russia vimeripoti kuwa shehena ya silaha za magaidi zimenaswa katika mkoa wa Homs nchini Syria; silaha ambazo imebainika kuwa ziliundwa katika nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato).

Andrei Nikpulov msemaji wa kituo cha Russia kinachohusika na mapatano ya pande zinazozozana huko Syria amesema kuwa shehena hiyo ya silaha imenaswa katika makao ya zamani ya kundi la kigaidi la Jabhatul Nusra katika eneo la Zaafaran nchini Syria.  

Silaha za magaidi zilizonaswa huko Homs, Syria 

Msemaji huyo ameongeza kuwa silaha na zana nyingi za kivita zilizonaswa zimeundwa katika nchi wanachama wa muungano wa Nato na kwamba magaidi walikuwa wameacha silaha nyingi za kisasa na zana za kijeshi katika ghala hilo. 

Silaha zote hizo ambazo zilitelekezwa na magaidi baada ya kujisalimisha kwa jeshi la Syria na kuelekea katika maeneo mengine zinajumisha aina mbalimbali ya silaha yakiwemo makombora na nyingine za kulenga vifaru aina ya Tau-2.  Ni miaka saba sasa ambapo Syria inakabiliwa na hali ya mgogoro na vita vya ndani vilivyosababishwa na uingiliaji wa Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu na Magharibi; na hadi kufikia sasa makumi ya raia wa nchi hiyo wameuawa na mailioni ya wengine kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi na hujuma za magaidi.  

Tags

Maoni