Mei 21, 2018 14:57 UTC
  • Hizbullah: Saudia inaumia kuiona harakati hii ikijumuishwa katika serikali mpya ya Lebanon

Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, amesema kuwa viongozi wa utawala wa Aal-Saud wanaumia mno kuona harakati hiyo ikijumuishwa katika serikali mpya ya Lebanon na kwamba viongozi hao ni madhaifu sana kuweza kuizuia Hizbullah kuingia serikalini.

Sheikh Nabil Qaouk amesema kuwa Lebanon haipo tayari kuathiriwa na malengo ya Saudia dhidi ya muqawama na amesisitiza kuwa, Hizbullah yenye nguvu itaingia katika serikali mpya ya nchi hiyo. Amezidi kufafanua kwamba, kama ambavyo viongozi wa Saudia walivyoingilia katika uchaguzi wa bunge uliopita, hata katika kuundwa serikali pia wanaingilia mambo ya ndani ya Lebanon kwa kuunda mirengo ya bunge dhidi ya muqawama. 

Sheikh Nabil Qaouk, Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah

Mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah amesema kuwa muqawama na baada ya mafanikio makubwa ya kisiasa uliyoyapata katika uchaguzi wa bunge umeendelea kuwa imara na wenye nguvu zaidi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto na hatari zozote zinazoukabili. Sheikh Nabil Qaouk ameongeza kwa kusema kuwa, mpango wa Marekani unaoitwa 'Muamala wa Karne' mbali na kwamba ni hatari kwa taifa la Palestina, ni hatari pia kwa Lebanon na kwa ajili hiyo ni lazima nchi hiyo ya Kiarabu iweze kupata nguvu ya kisiasa na kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na Washington dhidi ya Palestina na eneo.

Watawala wa Saudia ambao wanaumia kuiona Hizbullah inazidi kufanikiwa Lebanon

Kwa mujibu wa nyaraka za kuaminika, mpango huo wa Marekani unaoitwa 'Muamala wa Karne' mji wa Quds na matukufu yake unatakiwa kukabidhiwa utawala khabithi wa Israel na kwamba wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi nchi mbalimbali hawatakiwi kurejea makwao daima. Mbali na hayo ni kwamba ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Mto Jordan, unatakiwa kuendelezwa na Israel na kwamba Wapalestina watatakiwa kusalia tu katika eneo dogo la Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.

Tags

Maoni