Mei 23, 2018 03:31 UTC
  • Waziri Mkuu wa Iraq atoa amri ya kufuatiliwa magaidi wa Daesh nje ya mipaka ya Iraq

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitizia ulazima wa kudhaminiwa usalama wa mipaka ya nchi hiyo na kufanyika operesheni dhidi ya wafuasi wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nje ya mipaka ya Iraq.

Ofisi ya habari ya Haider al-Abadi, imesema kuwa kiongozi huyo wa Iraq alitoa amri hiyo wakati alipotembelea kamandi ya operesheni za pamoja za usafishaji wa nchi hiyo kutokana na uwepo wa magaidi wa kundi hilo sambamba na kufuatiliwa makundi mengine yenye mfungamano na magaidi. Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa, ni suala la dharura kuzuia upenyaji wa makundi ya kigaidi katika mipaka ya Iraq.

Haider al-Abadi, Waziri Mkuu wa Iraq

Kadhalika ametaka kufanyika operesheni na mashambulizi dhidi ya magenge hayo ya kigaidi nje ya taifa hilo. Kabla ya hapo ndege za kivita za Iraq zilishambulizi ngome kuu ya kundi la Daesh na waungaji mkono wake kusini mwa eneo la al-Dashishah katika ardhi ya Syria, ambapo katika operesheni hiyo ngome hiyo ilisambaratishwa kikamilifu. Habari nyingine zinaripoti kwamba, jeshi la Iraq limefanikiwa kusambaratisha njia kuu ya chini ya ardhi iliyokuwa ikitumiwa na magaidi wa Daesh (ISIS) mjini Mosul, kaskazini mwa Iraq.

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh

Kwa mujibu wa habari hiyo, kulikuwa na baadhi ya wanachama wa kundi hilo ndani ya njia hiyo. Kufuatia kushindwa vibaya kundi la Daesh nchini Iraq na Syria, wanachama wa kundi hilo waliosambaratika wameweka kambi katika mipaka ya nchi hizo suala ambalo limeyafanya majeshi ya nchi hizo (Iraq na Syria) kuanzisha operesheni kabambe kwa ajili ya kuyasafisha maeneo hayo ya mipakani.

Tags

Maoni