Mei 25, 2018 03:19 UTC
  • Netanyahu na Lieberman wafutiwa kibali cha kuanzisha vita bila ya idhini ya baraza la mawaziri

Baraza la Usalama la utawala wa Kizayuni wa Israel limebatilisha kibali alichokuwa amepewa waziri mkuu na waziri wa vita wa utawala huo cha kuanzisha vita dhidi ya nchi yoyote ile bila ya kupata idhini ya baraza la mawaziri.

Baraza la Usalama la utawala haramu wa Israel limeupigia kura za 'ndiyo' uamuzi wa kubatilisha sheria ambayo ilikuwa inampa idhini Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu, na waziri wake wa vita Avigdor Lieberman kujichukulia uamuzi peke yao wa kuanzisha vita katika hali ya hatari.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeashiria kufutwa kwa sheria hiyo ya kuanzisha vita na kusisitiza kuwa bunge la utawala huo Knesset ndilo lenye ustahiki wa kuchukua uamuzi juu ya suala hilo.

Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset

Sheria ya kuanzisha vita imebatilishwa baada ya makundi na mirengo mbalimbali kuikosoa sheria hiyo ambayo ilipendekezwa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.

Hapo kabla, na licha ya upinzani wa kamati za utaalamu, bunge la utawala haramu wa Israel Knesset lilimpa mamlaka waziri mkuu wa utawala huo kwamba katika hali ya hatari anaweza kutangaza vita dhidi ya nchi yoyote pasina kupata idhini ya baraza la mawaziri isipokuwa kwa kuitisha kikao cha masuala ya usalama kitakachohudhuriwa na waziri wa vita pekee.../

Tags

Maoni