Mei 26, 2018 02:21 UTC
  • Answarullah: Gharama za makombora yetu ziko chini kuliko za makombora ya Patriot ya Saudia

Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen amesema kuwa, gharama ambazo zimetumiwa na Wayemen kwa ajili ya kupata makombora ya nchi hiyo, ni chini ya gharama za fedha zinazotumiwa na Saudia kwa ajili ya kupata makombora ya Patriot.

Mohammed Ali al-Houthi sambamba na kusisitiza juu ya kufeli malengo ya wavamizi wa Saudia dhidi ya Yemen amesema kuwa, ubunifu wa Harakati ya Answarullah katika kusitisha mashambulizi yake ya makombora mkabala wa kukomeshwa pia mashambulizi ya kivamizi ya ndege za kivita za Saudia, ni wenye lengo la kuionyesha dunia kwamba harakati hiyo ina malengo ya amani.

Makombora ya Yemen ambayo jeshi la nchi hiyo likuwa likiyatumia kuishambulia Saudia

Ameongeza kwamba, raia wa Yemen kwa izza na utukufu wameweza kusimama imara kwa miaka kadhaa sasa kuhusiana na hujuma za Marekani, Saudia na washirika wake dhidi ya nchi hiyo katika hali ambayo nchi zote ambazo zinaizingira Yemen wananchi wao wanalia kutokana na ughali wa maisha na kushuka thamani ya sarafu yao. Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen amesema kuwa matatizo yanayolikumba taifa la Yemen kwa sasa yanatokana na mzingiro wa nchi za Kiarabu ambazo zinatumikia malengo machafu na njama za Marekani na utawala haramu wa Kizayuni. 

Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen

Kadhalika Mohammed Ali al-Houthi ameelezea mpango wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala katili wa Israel wa kulidhibiti kikamilifu lango la Bab-el-Mandeb na kusema kuwa mpango huo ni hatari sana. Amefafanua kuwa hivi sasa Saudia na Israel zinasaidiana katika maslahi na kwamba tawala hizo zinashirikiana kwa ajili ya kudhibiti njia zote za baharini za Yemen. 

Maoni