• Magaidi wazidi kutwangana Syria, zaidi ya 100 wauana kwa umati

Zaidi ya magaidi 100 wameuawa kaskazini na kaskazini magharibi mwa Syria katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika kwenye kipindi cha chini ya miezi miwili iliyopita.

Mtandao wa habari wa al 'Ahd wa nchini Lebanon umetangaza habari hiyo leo Jumapili na kuongeza kuwa, mapigano makali yaliyozuka baina ya magenge ya kigaidi ya Tahrir al Sham, Faliq al Sham, Jabhat Tahrir Suriyyah na Jaysh al Ghazzah katika kipindi cha siku 52 zilizopita kwenye mikoa ya Halab, Idlib na Hama huko kaskazini na kaskazini magharibi mwa Syria yamepelekea makumi ya magaidi kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Baadhi ya magaidi waliouawa katika mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe ni raia wa nchi za kigeni.

Ni jambo la kawaida kwa magenge ya kigaidi kushambuliana na kuuana kwa ajili ya kugombania maeneo wanayoyakalia kwa mabavu huko Syria

 

Habari nyingine kutoka Syria zinasema kuwa, "Kituo cha Upatanishi cha Russia" katika kituo cha kijeshi cha Hamim nchini humo kimesema kuwa, kambi ya wakimbizi ya al Rukban ya kusini mwa Syria imegeuka kuwa kimbilio na maficho makubwa ya magaidi.

Kambi ya wakimbizi ya al Rukban iko katika mpaka wa Syria na Jordan na hivi sasa inatumika kutoa mafunzo na kukusanya magaidi wakiwemo magaidi wa Daesh (ISIS) kwa ajili ya kufanya jinai nchini Syria.

Kambi hiyo iko umbali wa kilomita 300 kusini mashariki mwa mji wa Homs na iko karibu na kambi ya kijeshi ya Marekani. 

Tags

Jun 17, 2018 15:13 UTC
Maoni