Jun 18, 2018 07:27 UTC
  • Kamanda mmoja wa Saudia aangamizwa katika fukwe za magharibi mwa Yemen

Hussein Bokhami, mmoja wa makamanda wa Saudi Arabia pamoja na wanajeshi wengine kadhaa waliokuwa pamoja naye wameangamizwa katika shambulizi la jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen katika fukwe za magharibi mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo ikinukuu duru za kijeshi katika bandari ya al Hudaydah zikithibitisha habari hiyo na kuongeza kuwa, jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wanachi vimeshadidisha mashambulizi yao dhidi ya askari vamizi wa muungano wa Saudi Arabia na kuua makumi ya wavamizi hao na kujeruhi mamia ya wengine katika fukwe za magharibi mwa Yemen.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hivi sasa wanamgambo wa muungano wa Saudi Arabia wamezingirwa katika maeneo matatu ya magharibi mwa Yemen na hawana mawasiliano yoyote na wavamizi wenzao.

Wanajeshi vamizi wa muungano unaoongozwa na Saudia na Imarati wamepata hasara kubwa nchini Yemen

 

Huku hayo yakiripotiwa, jana jioni ndege za Marekani na Saudia ziliushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa al Hudaydah kwa zaidi ya mara 20.

Muungano wa baadhi ya nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia na Imarati kwa baraka kamili za nchi za Magharibi hasa Marekani na dola pandikizi la Israel, ulianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya mji wa bandari wa al Hudaydah wa magharibi mwa Yemen tarehe 13 mwezi huu wa Juni, ingawa hayo si mashambulizi ya kwanza kufanywa na wavamizi hao makatili katika mji huo.

Mashambulizi ya kiuadui ya wavamizi hao yanafanyika dhidi ya Waislamu wa Yemen licha ya jamii ya kimataifa kutahadharisha sana kuhusu hali mbaya ya kibinadamu iliyosababishwa na uvamizi wa Saudia na genge lake huko Yemen. 

Maoni