Jun 23, 2018 14:07 UTC
  • Gazeti la Kizayuni lafichua kikao cha Mohammad Bin Salman na Netanyahu

Gazeti la utawala haramu wa Kizayuni la Maariv limefichua kikao cha Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel nchini Jordan.

Jackie Hogi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa gazeti hilo amefichua kuwa, kikao cha siri kati ya Bin Salman na Netanyahu kilifanyika siku ya Jumatatu iliyopita katika safari aliyoifanya waziri mkuu huyo wa Israel mjini Amman, mji mkuu wa Jordan. Kwa mujibu wa Hogi ambaye ni mchambuzi wa masuala ya Kiarabu, mmoja wa marafiki wake wa karibu na ambaye alishiriki katika kikao hicho alimfahamisha kwamba Bin Salman alifanya vikao kadhaa kwa kuhudhuriwa na Mfalme Abdullah II wa Jordan na kadhalika vikao vingine kati yake na Netanyahu bila kuhudhuria mfalme huyo wa Jordan. Jackie Hogi ameongeza kwamba mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia alikutana na waziri mkuu wa Israel katika kasri la mfalme wa Jordan na pambizoni mwa vikao vya hivi karibuni  vya Jared Kushner na Jason Greenblatt, wajumbe wa Rais Donald Trump wa Marekani nchini Jordan.

Jason Greenblatt na Jared Kushner, wajumbe maalumu wa Rais Donald Trump wa Marekani katika nchi za Kiarabu

Wiki iliyopita Kushner na Greenblatt walifanya safari katika eneo la Mashariki ya Kati kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi za Kiarabu kwa ajili ya kufuatilia mpango wa njama ya Marekani dhidi ya Palestina unaoitwa 'Muamala wa Karne' ambapo hadi sasa wamesafiri Jordan, Misri, Saudia na Qatar. Saudia na katika kupenda kwake kujitanua imekwama katika kinamasi kufuatia migogoro iliyoianzisha eneo la Mashariki ya kati na katika uwanja huo badala ya kuimarisha mahusiano na nchi rafiki za Kiarabu na Kiislamu imekuwa ikifanya mahusiano ya siri na ya wazi na utawala haramu wa Israel ambao ni adui namba moja wa Waislamu duniani.

Tags

Maoni