Jun 24, 2018 01:14 UTC
  • Wakazi wa Al Hudaydah wawashukuru wapambanaji wa Yemen dhidi ya wavamizi wa Saudia

Katika kulaani mashambulizi ya wavamizi wa muungano wa Saudia na washirika wake, wakazi wa mkoa wa Al Hudaydah nchini Yemen wamefanya maandamano makubwa mjini hapo katika kuwapongeza wanamapambano wa nchi hiyo dhidi ya askari vamizi.

Washiriki wa maandamano hayo wamepiga nara za kupinga ukoloni na uvamizi wa Saudia na wakati huo huo kuunga mkono muqawama na mapambano ya jeshi la Yemen kwa kushirikiana na wanamuqawama wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah. Aidha washiriki wa maandamano hayo wamepongeza juhudi za makabila tofauti ya Yemen za kuiunga mkono mirengo kadhaa ya kimapambano na ushujaa wa raia wa nchi hiyo dhidi ya muungano vamizi wa Saudia na washirika wake ndani ya nchi hiyo.

Bandari ya Al-Hudaydah ambayo wavamizi wa Saudia, Israel, Marekani nk wanaikodolea macho

Muungano vamizi wa nchi za Kiarabu dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudia ulianzisha mashambulizi makali ya ardhini, baharini na angani dhidi ya mji wa Al Hudaydah kwa lengo la kudhibiti bandari na uwanja wa ndege wa mji huo. Hata hivyo njama hizo zimefelishwa na muqawama wa Answarullah na jeshi la Yemen.

Maoni