• Jeshi la Iraq laangamiza magaidi 45 wa Daesh Syria

Shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la Iraq limeangamiza wananchama 45 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika mkoa wa Dayr al-Zawr, mashariki mwa Syria.

Operesheni hiyo ya pamoja na jeshi la Syria lilifanywa jana Jumamosi kwa amri ya Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi.

Duru za kijeshi zinasema kuwa, naibu waziri wa vita wa Daesh, mmoja wa wakuu wa vitengo vya vyombo vya habari vya kipropaganda vya genge hilo, na mpambe wa karibu wa Abu Bakar Baghdadi, kiongozi wa kundi hilo la ukufurishaji ni miongoni mwa magaidi waliouawa katika operesheni hiyo ya jana katika eneo la Hajin.

Haya yanajiri katika hali ambayo, jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa vijiji vya al-Bustan na al-Shumariya katika mkoa wa Dara'a, mashariki mwa nchi toka mikononi mwa magaidi.

Hujuma ya anga dhidi ya ngome ya Daesh mkoani Dayr al-Zawr

Itakumbukwa kuwa Marekani na washirika wake waliunda muungano wa kimaonyesho kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) mwaka 2014, muungano ambao tangu kuundwa kwake umejikita tu katika kuishambulia miji ya Syria na kuwalenga askari wa serikali na raia wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Mara kwa mara serikali ya Damascus imekuwa ikipinga uwepo wa jeshi la Marekani ndani ya ardhi ya Syria na kuutaja kuwa ni uvamizi dhidi ya nchi huru. 

 

Tags

Jun 24, 2018 07:07 UTC
Maoni