Jul 11, 2018 04:26 UTC
  • Saudia yaendeleza tuhuma zake dhidi ya Iran

Serikali ya Saudi Arabia sambamba na kutuma barua kwenda Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imeituhumu nchi hii kwamba inakiuka haki yake ya kujitawala katika maji ya bahari ya nchi hiyo.

Katika barua hiyo, Saudia imedai kwamba boti na meli za Iran zimekuwa zikikiuka mipaka ya maji ya baharini kati ya nchi mbili. Inafaa kuashiria kuwa, Saudia kwa kushirikiana na Marekani na kwa muda sasa zimekuwa zikibuni na kueneza tuhuma za uongo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hii ni baada ya Iran kuwa na nafasi kubwa katika kuzima njama na hatua chafu za Marekani, Saudi Arabia na utawala haramu wa Kizayuni katika eneo la Mashariki ya Kati.

Pande tatu kuu katika kupanga njama chafu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Hayo yanajiri katika hali ambayo, kwa mara kadhaa boti za wavuvi wa Saudia na nchi nyingine za Kiarabu zimekuwa zikivuka maji ya Saudia na kuingia maji ya Iran huku maafisa usalama wa nchi hii wakiwakabidhi kwa nchi zao bila tatizo. Aidha miongoni mwa madai ya uongo ambayo yamekuwa yakitolewa na Saudia dhidi ya Iran ni kudai kwamba, Tehran imekuwa ikiingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine za Kiarabu, suala ambalo limekuwa likikanushwa mara kwa mara na viongozi wa nchi hii.

Tags

Maoni