• Mossad yakiri kushirikiana na kundi la kigaidi la MKO kula njama dhidi ya Iran

Shirika la Ujasusi la Utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD limejitokeza hadharani na kukiri kuhusu ushirikiano wake na kundi la kigaidi la MKO, kupanga njama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tovuti ya Israel ya Headshot imeripoti kuwa, Mossad ilikuwa imepanga njama na MKO juu ya kutekelezwa shambulizi la kigaidi dhidi mkutano wa kundi hilo la kigaidi mjini Paris, Ufaransa na kisha kuisingizia Iran kuwa ndiyo iliyohusika.

Mossad imedai kwamba, ilishirikiana na mashirika mengine ya kijasusi katika ya Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani kufichua 'mtandao wa kigaidi' uliokuwa unataka kushambulia Kongamano la MKO mnamo Juni 30. Mossad inadai kuwa mtandao huo ulikuwa ukiongozwa na mwanadiplomasia wa Iran katika mji mkuu wa Austria, Vienna, pamoja na raia wawili wa Ubelgiji na mmoja wa Ufaransa.

Washukiwa wote hao akiwemo mwanadiplomasia wa Iran na mkewe, walikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa tuhuma bandia za ugaidi.

Mkuu wa kudi la kigaidi la MKO, Maryam Radjavi, na aliyekuwa Meya wa York City Rudy Giuliani mjini Paris, Juni 30

Mwezi uliopita, Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kisiasa aliilalamikia serikali ya Ufaransa kwa kuwafadhili, kuwahami na kuwaruhusu magaidi wa MKO kufanya shughuli zao nchini humo licha ya magaidi hao kuwa na historia chafu ya kufanya ugaidi ndani na nje ya Iran.

Wataalamu kadhaa wa nyuklia wa Iran wameuawa shahidi na maajenti wa Mossad, wakiwemo Ali Muhammadi, Majid Shahriari, Dariush Rezaei Nejad, na Mostafa Ahmadi Roshan. 

Tags

Jul 20, 2018 14:10 UTC
Maoni