• Nyaraka za ushahidi wa msaada wa silaha wa Saudia kwa magaidi nchini Syria

Gazeti la Independent la Uingereza limechapisha nyaraka zinazoonyesha namna ambavyo Saudi Arabia imekuwa ikiwapatia silaha magaidi nchini Syria.

Katika taarifa ya Ijumaa, gazeti la Independent limeonyesha namna Saudi Arabia imekuwa ikiwatumia silaha magaidi wakufurishaji nchini Syria wakiwemo magaidi wa ISIS. Silaha hizo zimetengenezwa Marekani na zingine zimetengenezwa nchini Bosnia Herzegovina, Serbia na Bulgaria.

Saudia ilikuwa imenunua silaha hizo kwa njia rasmi kwa ajili ya kutumiwa na jeshi lake lakini ilikiuka taratibu na kuzikabidhi kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.

Tokea mwaka 2011, Syria imekuwa ikikabiliana na mashambulizi ya makundi ya magaidi wakufurishaji na wanamgambo wanaopata himaya ya kigeni, hasa Marekani na Saudi Arabia.

Magaidi wa ISIS

Katika miezi ya hivi karibuni, jeshi la Syria, likipata msaada wa waitifaki wake limefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa magaidi nchini humo. Mwezi Novemba mwaka jana, kwa msaada wa washauri wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, uungaji mkono wa vikosi vya Hizbullah na ndege za kivita za Russia, Jeshi la Syria lilifanikiwa kuukomboa mji wa Bukamal wa kusini mwa mkoa wa Deir ez Zor mashariki mwa nchi hiyo.

Eneo hilo lilikuwa ngome ya mwisho iliyokuwa ikidhibitiwa na magaidi wa ISIS. Baada ya kukombolewa mji huo, magaidi wa ISIS hawakua tena na ardhi waliyokuwa wameiteka nchini Syria. Hivi sasa Jeshi la Syria linaendeleza oparesheni zenye mafanikio za kuangamiza makundi mengine ya kigaidi nchini humo.

 

Tags

Jul 21, 2018 07:12 UTC
Maoni